Home Uncategorized Prof. Kabudi: Natamani Wabunge Tusiitwe Waheshimiwa

Prof. Kabudi: Natamani Wabunge Tusiitwe Waheshimiwa

77
0
Prof. Kabudi:Mbunge wa
Viti maalum (CUF), Riziki Shahari, amesema kero nyingi zilizopo nchini zingeondolewa
endapo mchakato wa Katiba mpya ungekamilishwa.

Waziri wa Katiba na
Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi amemjibu kwamba atahakikisha maoni yaliyokusanywa na
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, yanapewa uzito unaostahili kwasababu ndiyo
matakwa ya wananchi.
Amesema hata sasa baadhi ya maoni
hayo yanazingatiwa na Serikali ya Awamu ya Tano.
“Walitaka safari za viongozi
ziwekewe ukomo na malengo yake yawekwe wazi, bila shaka linaonekana
linavyozingatiwa, walitaka viongozi baada ya kuapishwa, wale kiapo kingine cha Maadili
ya Viongozi wa Umma nalo linafanyika.” Amesema Prof. Kabudi
Amesema yeye anapenda zaidi
pendekezola wananchi linalotaka wabunge na viongozi wengine wasiitwe Mheshmiwa, badala
yake waitwe Ndugu hali itakayoondoa  matabaka na kukweza viongozi dhidi ya wananchi wanaowaweka madarakani.
Hata hivyo amekiri kuwa wengi walichotaka ni taifa kuandika Katiba upya, jambo ambalo hata serikali inatambua umuhimu wake, lakini inaamini Katiba siyo kitabu.
Huku akiwa ameinua mkono wake wa
kuume ulioshikilia nakala ya Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977, amesema; “Zipo nchi hazina katiba
iliyoandikwa…, ukiuliza Waingereza katiba yao ni nini, utajibiwa ni Mila na Desturi, Israel
haina katiba iliyoandikwa, Zanzibar tangu ipate Uhuru hadi Mwaka 1977 haikuwa
na Katiba iliyoandikwa.”
Anaamini katiba ni jumla ya maisha
yote ya watu, ni matamanio, matarajio, shida na matakwa yao.
Akiwa ameinua tena Katiba hiyo akasema,
“Hii ambayo Waingereza hawana na wala hawaitaki…, sijui niyaseme tu kwakuwa sasa mimi ni waziriii?, walituandikia  wakiamini
hatuna mila na desturi zinazostahili kuwa Katiba.”
Hayo yamejiri kwenye mjadala wa hotuba
ya bajeti ya wizara hiyo, ya Mwaka 2017/18.