Home Uncategorized Maafisa Ununuzi Mpwapwa, Wanyooshewa Vidole

Maafisa Ununuzi Mpwapwa, Wanyooshewa Vidole

85
0Betri
ya gari N70 ambayo bei yake ni kati  ya Sh. 150,000 na Sh. 170,000
Halmashauri ya Mpwapwa inainunuwa kwa Sh. 320,000.

 

Hayo
yameelezwa na Diwani wa Kata ya Mazae, William Vahaye kwenyeKikao cha Baraza la
Madiwani wa Halmashauri hiyo, ambapo amesema anaamini kuna mchezo mchafu
unaoendelea kati ya baadhi ya watumishi wa halmasahauri na wazabuni.

Hatahivyo
Diwani mwingine wa Kata ya Lumuma, Jocktan Cheliga amesema inawezekana wazabuni
wanauza huduma na au bidhaa zao kwa bei kubwa, kutokana na halmashauri hiyo
kutekeleza shughuli zake nyingi kwa mkopo, kutokana na kukabiliwa na ukata.

Lakini
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Donart Ngwezi amesema kuna viashiria
kwamba wataalamu wa ununuzi wanatumia uelewa mdogo wa madiwani kuhusu sheria za
manunuzi, kuidhoofisha halmashauri.

Amesema
ingawa vielezo vyote vinaonesha kazi zinafanyika kwa kuzingatia taratibu,
anaamini kuna mchezo mchafu unaohusisha baadhi ya maofisa wa Idara ya Manunuzi.

Ameomba
na Baraza limeafiki kumuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Mohamed
Maje aandae semina elekezi kwa madiwani ili wajengewe uelewa wa Sheria ya
Manunuzi ya Mwaka 2011 na Kanuni zake.