Home Uncategorized Mgambo, Mtendaji wa Kata ya Mlowa Bwawani, Mbaroni Kwa Rushwa. Watuhumiwa Kuuza...

Mgambo, Mtendaji wa Kata ya Mlowa Bwawani, Mbaroni Kwa Rushwa. Watuhumiwa Kuuza Mbuzi 10 za Waliyemweka Mahabusu, Ili Fedha za Kuwahonga Zipatikane.

113
0
Sosthenes Kibwengo:
Mkazi
wa Kijiji cha Wiliko,Samwel Chilulumo, atakuwa mmoja wa mashahidi dhidi ya Mtendaji
wa Kata ya Mlowa Bwawani, Luis Pearson (37) na Mgambo wa Kijiji cha Mlowa
Bwawani, Josphat Msambili (37) wanaotuhumiwa kwa kushawishi na kupokea rushwa
ya Sh. 400,000.
Mkuu
wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa [TAKUKURU] wa Mkoa wa Dodoma,
Sosthenes Kibwengo, amesema Pearson na Msambili walimweka Chilulumo kwenye mahabusu
ya Kata hiyo, kwa Siku Mbili huku wakimshawishi awape Sh. 600,000 ili wamwachie
huru.
Amesema
Chilulumo aliomba kupunguziwa, nao wakapunguza mpaka Sh. 400,000 lakini alipowaomba
wamwachilie ili akawatafutie fedha hiyo walimkatalia.
Amesema
badala yake Msambili alikwenda kutafuta mteja wa Mbuzi zilizokuwa nyumbani kwa Chilulumo
na alipompata akawakutanisha, wakakubaliana bei na jumla ya Mbuzi Kumi
wakanunuliwa na mteja huyo ambapo malipo yalikabidhiwa kwa Msambili pamoja na Pearson.
Ikumbukwe; mwanzoni mwa
mwezi huu TAKUKURU watoa taarifa yao ya utendaji ya robo ya tatu na nne ya
mwaka huu, ambapo Sekta ya Serikali za Mitaa ilitajwa kuwa ya Pili ikiongoza
kwa kulalamikiwa na wananchi, ikiongozwa na Sekta ya Ardhi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo,
Sekta ya Serikali za Mitaa inalalamikiwa kwa asilimia 31 [31%] ya malalamiko na
tuhuma zote zilizopokewa na TAKUKURU katika kipindi hicho huku Sekta ya Ardhi
ikilalamikiwa kwa asilimia 36 [36%].
Kwa
mujibu wa Kibwengo, Chilulumo anakuwa shahidi kwasababu ndiye aliyetoa taarifa hizo
ambazo walizifanyia uchunguzi; 

Kwamba ingawa mtoa na mpokea rushwa wote ni
wahalifu, hali inabadilika pale mmoja kati ya pande hizo mbili anapotoa taarifa,
zikachunguzwa na ukweli kuthibitika.