Home Habari DKT. NDUMBARO AZUNGUMZA NA BALOZI WA UJERUMANI NCHINI

DKT. NDUMBARO AZUNGUMZA NA BALOZI WA UJERUMANI NCHINI

342
0

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), amefanya mazungumzo na Balozi Mteule wa Ujerumani nchini Tanzania, Regine Hess.

Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Ujerumani ambao ulijengwa tangu enzi za Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Nchi hizo zina zimekuwa na ushirikiano kwa miaka mingi, katika nyanja za kiutamaduni, kiuchumi na afya. Pamoja na mengine, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wenye tija, katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), akimkaribisha Balozi Mteule wa Ujerumani, Regine Hess, katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), akizungumza na Balozi Mteule wa Ujerumani, Regine Hess, alipomtembelea katika Ofisi ndogo za Wizara hiyo jijini Dar es Salaam
Balozi Mteule wa Ujerumani, Regine Hess, akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), alipomtembelea na kufanya naye mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizarahiyo jijini Dar es Salaam.

PICHA ZOTE NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO, WIZARANI.