Home Habari PROF. KABUDI ATETA NA MWAKILISHI WA UNICEF, TANZANIA

PROF. KABUDI ATETA NA MWAKILISHI WA UNICEF, TANZANIA

243
0
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) Tanzania, Shalini Bahuguna, akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi katika Ofisi ndogo za Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa, la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini Tanzania, Shalini Bahuguna, ameahidi kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania, kuhakikisha haki za watoto zinaendelea kulindwa nchini.

Ahadi hiyo imetolewa wakati wa mazungumzo maalumu na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi (Mb), yaliyofanyika kwenye ofisi ndogo za Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam.

“Haki za watoto katika taifa ni muhimu sana, tutaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuhakikisha zinalindwa, ikiwa ni pamoja na kupatiwa mahitaji muhimu,” amesema Bahuguna.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi (Mb), akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) Tanzania, Shalini Bahuguna, katika Ofisi ndogo za Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.

Naye Waziri, Prof. Kabudi aliishukuru UNICEF kwa kuwa bega kwa bega na Tanzania, katika kufanikisha agenda zake za maendeleo endelevu ya kulinda, kukuza na kutunza haki za watoto inasadikiwa ndiyo taifa la kesho.

Alisema tangu Mwaka 2016, Tanzania kwa kushirikiana na UNICEF, imeboresha sekta za elimu, afya na maji kwenye mikoa mbalimbali ikiwemo, Dar es a Salaam, Mbeya, Iringa, Kigoma, Njombe na Songwe.

Shughuli nyingine ambayo kwa ushirikiano na shirika hilo imefanikiwa, imetajwa naye kuwa ni kupunguza

 

maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi nchini.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) Tanzania, Shalini Bahuguna akimkabidhi nakala ya Hati ya Utambulisho Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi (Mb), katika Ofisi ndogo za Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.

PICHA ZOTE NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO CHA WIZARA.