Home Uncategorized KUTOKA MASJID GADDAF FOUNDATION.

KUTOKA MASJID GADDAF FOUNDATION.

395
0
Kaimu Katibu wa BAKWATA wa Mkoa wa Dodoma, Ustadhi Almarhum Twaha Y. Mwaya, wa Tatu kulia(enzi za uhai wake).

 

Inaa Lillahi Wainnaa Ilaihi Raajiuun.(Sisi ni wa Allah na kwake Allah Tutarejea.)

Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Sheikh Mustafa Rajabu Shabani, kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislam (BAKWATA) Mkoa wa Dodoma, anatangaza kifo cha Kaimu Katibu wa Baraza hilo, ambaye pia alikuwa Katibu wa BAKWATA wa Wilaya ya Dodoma – Jiji, Ustadhi Twaha S. Mwaya.

Amesema kifo hicho kimetokea jana Januari 19, 2020  Saa Sita mchana kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General).

Sababu za kifo zimetajwa naye kuwa ni ugonjwa wa moyo ambao alidumu nao kwa muda mrefu na shinikizo la damu la kupanda (High blood pressure). Taratibu za mazishi zinafanywa.

Ratiba ya mazishi:

Mwili wa marehemu utaswaliwa Masjid Gadafi baada ya swala ya Al-Asri jioni ya leo (Jumatatu). Kisomo cha Qur’aan (Khitmah) kitaanza Saa 9:30(Tisa na nusu, Al-asri).

Mazishi yatafanyika kwenye makaburi ya kwa Mwatano, Mailimbili, jijini Dodoma.

Wabllahi Taufiq.