Home Dodoma 74 % WAJIFUNGULIA VITUO VYA AFYA NCHINI: WAZIRI UMMY

74 % WAJIFUNGULIA VITUO VYA AFYA NCHINI: WAZIRI UMMY

95
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Na WAMJW-Dodoma

Wajawazito 813,923 sawa na asilimia 74 wamejifungulia kwenye vituo vya afya nchini, kuanzia Julai hadi Desemba mwaka jana kati ya wajawazito waliotarajiwa, milioni 1.1

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa wizara hiyo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge, ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Leo.

Kwa upande wa mahudhurio ya klininiki, Waziri Ummy, amesema waliohudhuria katika kipindi hicho walikuwa wajawazito 797,803 sawa na asilimia 73.

Amesema walifanya mahudhurio ya kliniki manne na zaidi, kama mwongozo ulivyoelekeza.

“Wajawazito 886,810 sawa na asilimia 87.4 waliopatia kinga za malaria, dozi 2,844,174 sawa na asilimia 84.6 zilitolewa kwa wajawazito kwa ajili ya kuzuia upungufu wa damu (FEFOL),” amesema.

Kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, wizara ilihakikisha dawa muhimu za kuzuia na kutibu kifafa cha mimba, kupoteza damu baada ya kujifungua na dawa za kutibu magonjwa ya watoto, wenye umri chini ya miaka mitano zinapatikana kwa zaidi ya asilimia 85.