Home Uncategorized MACHINJIO YA MSALATO, YAWA KAA LA MOTO KWA JIJI LA DODOMA

MACHINJIO YA MSALATO, YAWA KAA LA MOTO KWA JIJI LA DODOMA

263
0
WAZIRI SIMBA CHAWENE.

Machinjio ya mdana wa Msalato, jijini Dodoma yaliyofungwa Oktoba mwaka jana kwa uchafu, yamekataliwa kufunguliwa huku Sh. mil. 22 zikiwa zimetumiwa katika kuyafanyia ukarabati.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene baada ya kuyatembelea jana-Januari 22 mwaka huu, amesema hayafungu kwasababu ukarabati uliyofanywa hauna viwango vya serikali.

“Nasema silifungui hili jengo lisilo na viwango vya kiserikali na nikiuliza fedha zilizotumika hapa inashangaza, hili ni sawa na jengo la mlala hoi,”amesema Simbachawene.

MKURUGENZI WA JIJI LA DODOMA, GODWIN KUNAMBI.Ametoa muda wa wiki moja kwa uongozi wa Jiji la Dodoma, kuhakikisha kasoro alizozibaini zinaondolewa.

Ikumbukwe Oktoba 2019 – miezi mitatu iliyopita, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) lilifunga machinjio hayo ambapo pamoja na hatua nyingine, halmashauri hiyo iliamriwa kulipa faini ya Sh. mil. 5(Milioni Tano).