Home Burudani SHILOLE KUGOMBEA UBUNGE JIMBONI KWA DKT. KAFUMU

SHILOLE KUGOMBEA UBUNGE JIMBONI KWA DKT. KAFUMU

276
0
MBUNGE WA IGUNGA, DKT. PETER KAFUMU

Msanii wa filamu na muziki nchini, Zuwena Mohamed ‘Shilole au Shishi baby’ ambaye pia ni mjasiriamali amesema atagombea ubunge wa Igunga, jimbo ambalo kwa sasa mbunge wake ni Dkt. Dalaly Peter Kafumu.

MSANII NA MJASILIAMALI, ZUWENA MOHAMED ‘SHILOLE’

Hata hivyo bila kutaja majina, amewataka wote ambao wameanza kuweweseka kwa taarifa za nia yake hiyo, kutulia kwakuwa alichofanya ni kutangaza jambo ambalo anatamani litokee maishani mwake.

Amesema hana haja ya kujenga mazingira ya kukubaliwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo, kwasababu ndiko ilipo asili yake, anafahamika vilivyo na wengi wamefurahia kusikia ana nia ya kuwa mwakilishi wao bungeni.

SHILOLE AKIWA KAZINI.

Amesema hakuwahi kuwa chama kingine cha siasa zaidi ya CCM na ametaja wanasiasa watatu wanawake, kwamba ndiyo wanaomvutia kiasi cha kuhisi anatakiwa kujiongeza katika ulimwengu wa kisiasa.

Amemtaja Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu pamoja na kijana mwanasiasa mwenye mvuto wa aina yake, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo.

Zuwena kando ya kumiliki na kufanya kazi kwenye mgahawa wake unaofahamika kwa jina la ‘Trump Food’ ameingiza sokoni sabuni anazotengeneza.