Home Habari MABALOZI WASIO NA MAKAZI NCHINI, WAJITAMBULISHA KWA PROF. KABUDI

MABALOZI WASIO NA MAKAZI NCHINI, WAJITAMBULISHA KWA PROF. KABUDI

109
0
Mkuu Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge (mwenye tai ya rangi ya chungwa), akiwapa semina mabalozi wateule, kabla hawajasilisha nakala za hati za utambulisho wao kwa Waziri wa Wizara hiyo, Prof. Palamagamba Kabudi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi
(Mb), akiangalia nakala ya hati ya utambulisho ya Balozi wa Ureno, Balozi Maria Amelia Maio de Paiva
Balozi wa Venezuele, Jesús Agustin Manzanilla Puppo akimfafanulia baadhi ya maneno yaliyopo kwenye nakala ya hati ya utambulisho, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb).
Balozi wa Jamaica, Angela Veronica Comfort akimkabidhi nakala ya hati ya utambulisho wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) akikagua nakala ya hati ya utambulisho ya Balozi wa Austria, Dkt. Christian Fellner.
2. Balozi wa Ufilipino, Alex G. Chua akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb), alipopatiwa ufafanuzi wakati wa mazungumzo, mara baada ya kumkabidhi waziri nakala ya hati ya utambulisho.
Balozi wa Ghana, Fransisca Ashietey-Odunton akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) nakala ya hati ya utambulisho wake.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi (Mb), akiangalia nakala ya hati ya utambulisho wa Balozi wa Djibouti, Yacin Elmi Bouh.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi (Mb), amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi Wateule wasio na makazi nchini.

Tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam.

Mabalozi hao ni wa Nchi za Ureno-Maria Amelia Maio de Paiva mwenye makazi jijini Maputo, Ufilipino-Alex G. Chua mwenye makazi jijini Nairobi, Jamaica-Balozi Angela Veronica Comfort mwenye makazi jijini Pretoria na Austria- Dkt. Christian Fellner ambae makazi yake yapo Nairobi.

Wengine ni Balozi wa Ghana-Fransisca Ashietey-Odunton mwenye makazi Jijini Nairobi, Venezuele-Jesús Agustin Manzanilla Puppo mwenye makazi jijini Nairobi na Djibouti-Yacin Elmi Bouh mwenye makazi Nairobi.

Awali kabla ya kukabidhi hati za utambulisho kwa Mhe. Waziri, Mabalozi wateule walipata semina kutoka kwa Mkuu wa Itifaki, wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge.

HABARI, PICHA ZOTE NA

KITENGO CHA HABARI

NA MAWASILIANO CHA WIZARA HIYO.