Home Dodoma CHUO CHA HOMBOLO KUONDOA VICHAKA, MAGOFU KWA RC DODOMA

CHUO CHA HOMBOLO KUONDOA VICHAKA, MAGOFU KWA RC DODOMA

270
0
WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI), SELEMAN JAFO.

ENEO lenye vichaka vya kutosha, katikati ya Jiji la Dodoma sasa litakuwa na mwonekano wa tofauti, baada ya serikali kuamua kujengwe Kampasi mpya ya Chuo cha Serikali za Mitaa – Hombolo.

Kiwanja hicho ni zilipokuwa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, kabla hazijateketea kwa moto, sehemu yake kubwa ikageuka vichaka na baadhi ya majengo yakawa magofu kwa miaka mingi.

MKUU WA MKOA WA DODOMA, DKT. BINILITH MAHENGE.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Seleman Jafo alitangaza uamuzi huo jana wakati akizindua Jengo la Makao Makuu ya Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) jijini humo.

SEHEMU YA KIWANJA HICHO KILICHO KWENYE MAKUTANO YA TAA ZA BARABARANI ZA JIRANI NA BAA YA CHAKO NI CHAKO.

Alisema alitarajia Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge, angekuwepo ili ampe maelekezo. Hatahivyo alisema uamuzi huo unatakiwa kutekelezwa mapema iwezekanavyo ili kuwarahisishia watumishi na viongozi kujiendeleza kitaaluma.

Waziri Jafo alimuuliza Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Mpamila Madale watajenga aina gani ya jengo na alijibiwa kuwa watajenga jengo lenye gorofa zisizopungua Tano.