Home Habari TANZANIA, INDONESIA KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA KWA NDEGE.

TANZANIA, INDONESIA KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA KWA NDEGE.

236
0
Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhani Kitwana Dau akimuonesha moja ya filamu za utalii, Balozi wa Indonesia nchini Malaysia, Rusdi Kirana.

BALOZI wa Indonesia nchini Malaysia, Rusdi Kirana ambaye pia ni mfanyabiashara mkubwa ameafiki kutumia mashirika yake ya ndege kutangaza utalii wa Tanzania bila malipo yoyote kutoka kwa Tanzania.

Balozi huyo anamiliki Mashirika ya Ndege ya Lions Group, Batik na Malindo, ataonesha filamu za kutangaza utalii wa Tanzania kwenye ndege, kupitia inflight entertainment.

Uamuzi huo ni matokeo ya mazungumzo kati yake na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Ramadhani Kitwana Dau, ambaye pia anawakilisha Indonesia.

Mashirika hayo yenye ndege zaidi ya 300 na wafanyakazi 43,000 yanahudumia abiria milioni 60 kwa mwaka (wastani wa abiria 160,000 kwa Siku) na zina Safari 3,400 kwenda na kurudi kila siku, kwenye nchi zaidi ya 50.

Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhani Dau akimkabidhi moja kati ya filamu za utalii Balozi wa Indonesia nchini Malaysia, Balozi Rusdi Kirana.

Mabalozi hao wamekubaliana kuwepo umuhimu wa kutangaza utalii katika ukanda wa Kusini Mashariki ya Asia, Balozi Kirana ameahidi kuanzisha Safari za ndege kati ya Indonesia na Tanzania, baada ya kufanya mazungumzo na mawakala wa utalii nchini humo.

Balozi Kirana ameukubali mwaliko wa Dkt Dau wa kutembelea Tanzania, ameahidi kufanya matembezi hayo katikati ya Septemba, Mwaka huu.

Baada ya mazungumzo hayo, amemkabidhi Balozi Dkt. Dau mfano wa ndege zake, kwa ajili ya kuzitumia kama mapambo ofisini.

HABARI, PICHA ZOTE NA;KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO CHA WIZARA.