Home Dodoma DKT. BASHIRU AMKABIDHI MSTAAFU MSAADA WA KINUKUZI

DKT. BASHIRU AMKABIDHI MSTAAFU MSAADA WA KINUKUZI

212
0
KATIBU MKUU WA CCM – TAIFA, DKT. BASHIRU ALI, (ALIYEVAA SARE YA CHAMA) AKIZUNGUMZA KWENYE MAKAO MAKUU YA CHAMA HICHO JIJINI DODOMA LEO.

KATIKA kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dkt. Bashiru Ally, amempa Shabani Kanijo (73), Kinukuzi (Photocopy machine) chenye thamani ya Sh. Milioni 1.5

Kanijo alikuwa mtumishi wa CCM, makao makuu kwenye Kitengo cha Tehama tangu mwaka 1965 hadi 2004, alipostaafu.

Awali akiwa Ofisini kwa Dkt. Bashiru, Kanijo alisema muda mchache baada ya kustaafu alishambuliwa na maradhi yaliyosababisha ashindwe kuendeleza biashara ya steshenari na hivyo kuishi bila chanzo maalum cha mapato.

Nacho CCM kwa kuzingatia utaratibu wake wa kuwa karibu na makundi mbalimbali ya jamii, hususan wazee, leo Februari 05, Mwaka huu Katibu Mkuu wake, Dkt. Bashiru amemkabidhi vifaa vyote vinavyohitajika kwenye biashara hiyo, ikiwamo mashine hiyo.

SHABANI KANIJO (73), AKIWA MAKAO MAKUU YA CCM, AMBAPO AMEPOKEA MSAADA WA KINUKUZI KUTOKA KWA DKT. BASHIRU, LEO.

Naye Kanijo, amekishukuru Chama hicho kwa kuendelea kuwa karibu na wazee na kwa utekelezaji wa Ilani uliotukuka, kwakuwa sasa hata wapinzania hawana ajenda  tena.

“Hao wapinzania watake nini tena? Kwakuwa hata mambo waliyokuwa wanayatak, yametimizwa na CCM inayoongozwa na Rais Magufuli,” amesema.

Kwa upande wa Dkt. Bashiru amesisitiza kuwa vifaa hivyo vimetolewa na Chama, itapendeza vitumike kwa malengo yaliotarajiwa ili desturi hiyo iendelee kunufaisha wengi zaidi, kadri ya mahitaji na uwezo wa Chama hicho.

Leo ni maadhimisho ya kumbukumbu ya siku kiliyozaliwa CCM, kikitimiza miaka 43 tangu kiundwe kwa kuunganisha Vyama vya TANU na ASP, Februari 05, Mwaka 1977.

IMETOLEWA NA SAID SAID NGUYA, AFISA HABARI, OFISI YA KATIBU MKUU, CCM.